Idadi Ya Waliofarilki Kutokana Na Pombe Haramu Kaunti Ya Nakuru Imeongezeka Hadi 7 Baada Ya Mtu Mmoja Kufariki Mapema Leo.Tukio Hili Limepelekea Wakaazi Wa Eneo La Njoro Waliojawa Na Ghadhabu Kuvamia Na Hata Kuteketeza Maeneo Yanayokisiwa Kuwa Ya Kutengeneza Pombe Hiyo. Kulingana Na Mshirikishi Wa Ukanda Wa Bonde La Ufa George Natembeya, Serikali Imeanzisha Operesheni Kali Dhidi Ya Wagema Hao.